Thursday, April 2, 2020

RC Tabora Awaagiza Kusakwa Na Kukamatwa Kwa Walimu Wanaofundisha Tuisheni Kipindi Hiki Cha Mapambano Dhidi Ya Corona


Na Daudi Tiganya
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kuwasakwa kwa walimu ambao wamekuwa wakiwakusanya wanafunzi kwa ajili ya kufundisha tuisheni kwa kuwa wanapingana na kampeni  ya kudhibiti na kupambana na  ugonjwa wa Covid -19.

Hatua hiyo inalenga kuzuia vitendo hatarishi vinavyoweza kuwepo na mazingira kupata virusi vya Corona.

Mwanri alitoa kauli hiyo  wilayani Nzega wakati ziara yake ya kukagua Vituo na Zahanati zilizoandaliwa kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa wa covid -19 kama itatokea bahati wakaonekana wakaonekana Mkoani humo.

Alisema ni marufuku kwa walimu kutumia janga la ugonjwa wa Covid -19 kujipatia maslahi kwa kufanya hivyo ni kuvunja Sheria kwa kisingizio kuwa wanawafundisha watoto masomo ya ziada.

Mwanri aliongeza kuwa baadhi ya Wamiliki wa Shule binafsi ndio wanasababisha walimu kujiingiza kwenye ufundishaji wa tuisheni baada ya kusema kuwa kuambiwa kuwa  hatawalipa mshahara kwa sababu hawakufundisha katika kipindi ambao shule zimefungwa kutokana na Covid -19.

Alisema hilo halikubaliki na ndio linalowafanya baadhi yao kujiingiza katika ufundishaji wa tuisheni kinyume cha maagizo ya serikali katika kukabiliana na Covid 19.

Mwanri alisema ni lazima walimu wote walipwe mshahara wao ili kutowaweka katika vishawishi vya kujiingiza katika kuvunja maagizo ya Serikali ya kuzuia mikusanyiko kwa wanafunzi.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honaratha Rutatinisibwa aliwataka wazazi kutowaruhusu watoto wao kuzuzura ovyo mitaani kwa kuwa vitendo vinaweza kuwasababisha kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Alisema kuna baadhi ya maeneo kunaonekana makundi ya watoto wakiwa wamekusanyika pamoja jambo ambalo ni hatari kwao na kwa jamii zinazowazunguka.

Dkt. Rutatinisibwa alisema ni vema wanafunzi wakasisitizwa kubaki majumbani katika kipindi hiki ambacho mapambano dhidi ya Corona yakiendelea
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...