Thursday, April 23, 2020
JPM: Barakoa Zikaguliwe, Tusije Tukaambukizwa Corona na ‘Mask’ Kutoka nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhakikisha wanakagua vifaa vyote vya kujikinga na corona vinavyoingia nchini.
Akizungumza na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, leo, Aprili 22, 2020, Rais Magufuli amesema kuwa katika nchi nyingine wametilia shaka baadhi ya misaada ikiwa ni pamoja na barakoa.
"Kuna nchi baadhi wameanza hata kuuliza hivi vifaa vya misaada ambavyo vinatumika. Na ndio maana nimeona nizungumze hili kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Wizara ya Afya waanze kushughulikia hata vitu tunavyopewa kama zawadi ili visije vikatuletea madhara," amesema Rais Magufuli.
"Unapoletewa mask ya kujikinga puani (barakoa) ni lazima tujue hiyo mask aliyeitengeneza, aliyei-supply na misingi ya kutuletea; kwa sababu la sivyo tunaweza tukajikuta tunaambukizwa corona kwa mask za kutoka nje," ameongeza.
Rais ametoa wito kwa taasisi na viwanda nchini kuanza kutengeneza barakoa huku akiwapongeza Watanzania ambao wamechukua hatua ya kuanza kushona wenyewe barakoa.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alishangaa utaratibu ulikuwa umeanza kuwekwa na Wizara wa kupuliza dawa 'fumigation' kwenye vyombo vya usafiri.
"Wizara ya Afya nimeambiwa siku za nyuma walitoa amri ya kufanya furmigation… mabasi yaende wapi yanafanyiwa fumigation, yakifika sokoni yanafanyiwa fumigation. Na hili Dar es Salaam nililiona sana na Mwanza, hakuna fumigation yoyote inayoweza kuua corona, na hili Watanzania ni lazima tuambizane ukweli," amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli alisema kuwa kama fumigation ingeweza kuua virusi vya corona, basi nchi zinazoendelea wangehakikisha wanamwaga kwenye maeneo yao yote kwakuwa wana uwezo huo.
Source
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
