Sisi tulifundishwa na kuaminishwa kuwa asili ya mwanadamu ni mnyama nyani.... Ni katika harakati za kutatua changamoto za maisha yanayomzunguka ndio akajikuta mpaka anaweza kusimama kwa miguu miwili na kutumia mikono kwa shughuli nyinginezo... Ithibati za kuunga zikionesha kutoka hatua za homo sapien mpaka homo habilis.. Ambaye sasa alikuwa ni binadamu kamili....
Kadiri tunavyozidi kuzama na kuhoji kuhusu hizi elimu na uhalisia wake ndivyo tunavyozidi kuangaziwa na kufunuliwa kuhusu uongo na upotoshaji mwingi kisayansi, kibaologia na kihistoria...
Ndana ya binadamu wa kwanza kutokana na nyani inawezekana kabisa ndio dhana dhaifu zaidi na inayoongoza kwa uongo na upotoshaji kuliko dhana nyingine zote kuhusiana na asili ya mwanadamu
Kuna maswali mengi ya kuhoji hapa
- Asili ya huyo nyani ni ipi?
- Kwanini baada ya hapo nyani wengine hawakupitia mchakato wa mabadiliko mpaka kuwa binadamu?
- Kwanini sasa nyani azae nyani na binadamu azae binadamu?
- Kwanini kusiwe na kinyume cha binadamu kuzaa nyani na nyani kuzaa binadamu?
Pamoja na mfanano wa vinasaba kati ya nyani na binadamu kwa zaidi ya asilimia 90.. Lakini ukweli unabaki kuwa hizi ni asili mbili tofauti kabisa
Dhana ya binadamu kubadilika umbo tangu kuumbwa kwa dunia inaweza kuwa na mashiko... Tukisoma misahafu tunaambiwa kuna watu waliishi zaidi ya miaka 800,Lakini pia kuna simulizi za wanefili, majitu makubwa yaliyoishi zamani...rejea zinjathropus
Kadiri miaka inavyosonga umri wa kuishi unazidi kupungua na hata maumbo pia.. Na hii si kwa binadamu tuu bali hata wanyama na vitu vingine vingi...
Dhana pekee ambayo mpaka sasa inajadilika ni Ile dhana ya uumbaji wa kiimani... Dhana ya asili ya mwanadamu na uumbaji wa kimungu...
Upotoshaji huu wa historia ulifanywa na watu maalum... Je lengo lao lilikuwa ninini?
Source