Friday, April 3, 2020

DC Katambi Ampa Siku 3 Masanja Mkandamizaji Kuripoti Ofisini Kwake Jijini Dodoma Baada Ya Kufanya Mzaha Juu Ya Corona

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini Mhe.Patrobas  Katambi amempa siku 3 Mwigizaji wa vichekesho Emanuel Mgaya[Masanja Mkandamizaji ]kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Dodoma baada ya kuleta Mzaha juu ya suala la Corona.

Akizungumza jijini Dodoma  mbele ya   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mkuu huyo wa wilaya mhe.Patrobas Katambi amesema Mwigizaji huyo, Emmanuel Mgaya [Masanja Mkandamizaji ]ambaye pia anafanya vipindi kupitia Shirika la Utangazaji Ujerumani [DW]akiwa Jijini Dodoma amefanya Mzaha juu ya ugonjwa wa Corona hivyo anatakiwa kuripoti ofisini kwa  mkuu wa wilaya Dodoma kujibu tuhuma kwanini analeta mzaha .

"Mhe.Mkuu wa Mkoa kuna jambo muhimu nimeliona ,ninakumbuka kwenye mkoa wako huu,pia Wilaya ya Dodoma viongozi wametuagiza tusifanye mzaha juu ya Ugonjwa huu wa Corona lakini cha kushangaza kuna mwigizaji pia anafanya kazi na shirika la Utangazaji Ujeruman [DW]anaitwa Masanja Mkandamizaji amefanya mzaha juu ya ugonjwa huu akiwa Dodoma akithibitisha kuwa watu wa Dodoma hawajui maana ya ugonjwa huo akitumia neon la kiingereza [COVID-19]kwa hiyo tunamwomba mtu huyu kufIkia Jumatatu afike hapa Dodoma atuambie malengo yake yalikuwa ni nini hasa "amesema Katambi.

Hivi Karibuni Emmanuel Mgaya[Masanja Mkandamizaji] akiwa makao  makao makuu ya nchi ya nchi wakati akifanya mahojiano na baadhi ya wananchi wakati akifanya kipindi chake kutoka DW aliwahoji wakazi wa Dodoma kuwa wanataka kuletewa COVID -19 ngapi ambapo bila ya kujua maana ya COVID 19 baadhi ya wananchi walisema   wanahitaji waletewe COVID 19  elfu tano[5,000].

Ikumbukwe kuwa COVID -19 ni ufupisho wa maneno ya Kiingereza "Corona Viruse Disease ambapo virusi hivyo viligunduliwa mwaka 2019 .


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...