Thursday, April 9, 2020

Baraza la Usalama la UN kujadili janga la virusi vya corona

Baada ya wiki kadhaa za kutoelewana -- hasa kati ya Marekani na China -- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo kujadili janga la virusi vya corona kwa mara ya kwanza.

Wakiongozwa na Ujerumani, tisa kati ya wanachama 10 wasio wa kudumu wa baraza hilo wiki iliyopita waliitisha kikao cha faragha -- mkutano wa video ili kuepuka kukaribiana -- baada ya kuchoshwa na ukosefu wa hatua kutoka kwa baraza hilo kuhusiana na mgogoro huu wa kimataifa usio wa kawaida.

Wanadiplomasia wamesema mazungumzo yako kwenye mkondo mzuri na Marekani haisisitizi tena kwamba lugha inayopaswa kutumiwa na Umoja wa Mataifa ionyeshe kuwa virusi hivyo vinatokea China, kitu ambacho kiliikasirisha China.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kulenga juhudi za kupambana na janga hilo, operesheni za kulinda amani na kukuza umoja kati ya wanachama wasio wa kudumu na watano ambao ni wa kudumu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...