Thursday, March 26, 2020

Mwanzilishi wa Mtandao wa Wiki akataliwa dhamana kuhusiana na virusi vya corona



Mwanzilishi wa mtandao wa kufichua nyaraka za siri wa Wikileak Julian Assange, ameshindwa katika jaribio lake la kuachiwa kwa dhamana, ambamo amedai anakabiliwa na hatari ya kuambukizwa virusi vya corona katika gereza anakoshikiliwa.

Jaji anayehusika na kesi hiyo Vanessa Baraitser amesema hali ya mripuko wa ugonjwa huo kwa sasa haikidhi vigezo vya Assange kuachiwa kutoka gerezani.

Assange anashikiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh Kusini mwa London, akiendeleza juhudi za kupinga kupelekwa nchini Marekani, ambako anakabiliwa na mashtaka ya ujasusi.

Jaji Baraitser amesema Assange tayari alivunja masharti ya dhamana, alipokimbilia katika ubalozi wa Ecuador mjini London mwaka 2012.

Uingereza inatafakari kuwaachia baadhi ya wafungwa kwa lengo la kupunguza msongamano magerezani, kupunguza hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...