Thursday, August 8, 2019

JKT Yaja na Habari Njema kwa Wananchi wa Kanda ya Kusini

JKT Yaja na Habari Njema kwa Wananchi wa Kanda ya Kusini
Wananchi wa mikoa ya Kusini( Lindi na Mtwara) wameombwa kutumia maonesho ya nane nane na  kanda ya ujenzi ya kanda ya Kusini kupata msaada wa kitaalamu wa mambo mbalimbali yahusuyo shuguli za maendeleo.

Wito huo ambao ni habari njema kwa wananchi wa kanda ya hii ulitolewa jana na Luteni Kanali Juma Mrai alipozungumza na Muungwana Blog katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi, yanapofanyika maonesho ya wakulima( Nanenane) kanda ya Kusini.

Luteni Kanali Mrai ambae amemuwakilisha mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) alipotembelea mabanda ya maonesho ya jeshi hilo wajifunze kupitia mambo wanayoyaona katika mabanda hayo, ili maonesho hayo yawanufaishe.

Katika maonesho hayo, alisema wananchi hawanabudi kutumia kanda hiyo ya ujenzi kupata ushauri wa kitaalamu katika shughuli zao za maendeleo na ujenzi wa taifa.

Alisema jeshi hilo ni mali yao na lipo kwa ajili yao, kwahiyo wana haki na sababu ya kulitumia, Ikiwemo kupata ushauri kuhusu kilimo, ufugaji, uvuvi na fani nyingine zinazoweza kuwafanya wanufaike na kazi wanazofanya.

Mbali na kutoa  ushauri, kamanda huyo alisema kanda  ya ujenzi ina toa huduma za ujenzi kwa taasisi za umma,taasisi binafsi na mtu mmoja mmoja. Hivyo wasisite kuwatumia katika kazi zao.

 ''Waendelee kuliamiani jeshi lao, kwani gharama za ujenzi ni nafuu, watakamilishiwa kazi zao kwa wakati, kwamujibu wa mikataba na kwa ubora,'' alisisitiza kamanda Mrai.

''Lakini pia wananchi wanapata fursa ya kuona vijana wao kupitia jeshi lao wanafanya nini. Kwani ni dhahiri wanapata ujuzi na maarifa yanayoweza kuwafanya wajiajiri,'' alisema kamanda Mrai.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...