Wednesday, August 21, 2019
Faida za kufanya mazoezi nyakati za asubuhi
Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa afya yako, kuna namna mbalimbali za kufanya mazoezi, Unaweza kufanya mazoezi ya viungo fulani vya mwili wako kama miguu, mikono, mgongo.
Lakini pia kuna mazoezi ambayo ukifanya utakuwa umefanya zoezi lilojumuisha kiungo zaidi ya kimoja mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo.
Licha ya kuwa unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni lakini pia unaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa kufanya mazoezi hayo.
Kwa kuwa kuna faida nyingi za kufanya mazoezi basi leo nimeona nikupatie hizi chache kwa manufaa na ufahamu wa afya yako.
Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa shupavu.
Mazoezi huboresha ufahamu wako uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.
Mazoezi huboresha uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu.
Mazoezi husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
Mazoezi huimarisha moyo hivyo hukuepusha na maradhi mengi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo.
Mazoezi humfanya mtu ajiamini.
Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia baridi.
Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini.
Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.
Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. (high blood pressure)
Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.
Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili.
Mazoezi huboresha hamu ya mtu kuweza kula.
Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.
Mpendwa msomaji hizi ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, yote ya yote mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya njema.
Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli ukifanya mazoezi na kula vyakula bora kunaweza kuboresha maisha yako? Jibu ni ndiyo mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika. Fanya mazoezi kuimarisha afya yako!
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...