Wednesday, June 19, 2019

Rasmi: KMC FC yamsajili Ismail Gambo



Klabu ya KMC FC imemsajili rasmi mchezaji Ismail Gambo kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomalizika mwezi Juni mwaka 2022.

Gambo alikuwa KMC kwa mkopo kutoka Azam FC na sasa ni mchezaji rasmi wa timu hiyo yenye jukumu la kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.

Klabu hiyo pia imewaongezea mikataba wachezaji wake Rehani Kibinga na Sadala Lipangile waliosaini mikataba mipya ya miaka mitatu kila mmoja hadi mwaka 2022.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...