Thursday, April 25, 2019
Zari Amtambulisha Mpenzi Wake Mpya ‘Mimi Huwa Nawajenga Wanaume Wangu’
Mfanyabiashara wa Uganda na mpenzi wa zamani wa nyota wa muziki wa bongo nchini Tanzania Diamond Platnumz, Zari Hassan amepata mpenzi mpya yapata mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu alipotangaza kuvunjika kwa uhusiano wake na mwimbaji huyo wa 'Zilipendwa na Hallelujah'
Mpenzi huyo mpya ambaye amemtaja kuwa Bwana 'M' katika mtandao wake wa Instagram ndiye aliyechukua mahala pake Diamond.
Akitangaza uhusiano wake mpya katika mtandao huo wa kijamii siku ya Ijumaa jioni, Zari Hassan alisema kuwa mpenzi wake mpya amemkubali yeye pamoja na watoto wake wote watano.
"Kwako wewe mpenzi nimejifunza mengi; Nakumbatia maisha yalivyo kwa sababu ya unyenyekevu wako. Nimekuwa nikifikiria maisha yangu ya baadaye lakini sikuweza kujua maisha hayo yatakuwa vipi. Watoto watano, wanaume wengine lakini bado ukaniona mimi kuwa mwanamke mrembo zaidi", alisema Zari katika chapisho lake ambalo limevutia majibu 100,000.
"Nakupenda sana bwana M, na sio vitu vyenye thamani unavyonionyesha, nimeviona hivyo na hata vikuu na vizuri zaidi. Lakini ni wewe, moyo wako, uwepo wako na vile unavyotufanya mimi na wanangu kukuhisi. Wewe ni jasiri sana bwana M: Watoto watano ; mimi mwenyewe nina umri wa miaka 38…wow…umetumwa kutoka mbinguni mpenzi. Nakupenda bwana M",aliongezea Zari katika chapisho hilo.
Mfanyabiashara huyo wa Uganda alizungumzia kuhusu nafasi yake katika kujenga maisha ya wapenzi wake wa awali ambao anasema hawakumpenda kwa dhati.
Zari hakusita kuwakemea wale wanaodai wanamjua mpenzi wake mpya katika ukurasa wake wa Facebook.
"Wacheni kile amabcho wanablogu wanachapisha lengo nlao ni kuvutia usomaji katika blogu zao", alisema.
"Mimi hupenda na huwajenga wanaume wangu, mimi sio mtu anayekusanya na kuondoka, mimi hutazama kile tulichokubaliana kwa lengo la kuongeza baraka", alisema.
Tangazo hilo limevunja matumaini ambayo wafuasi wa Zari Hassan na Diamond walikuwa nayo -kwamba siku moja pengine wawili hao watarudiana.
Ni wakati wa siku ya wapendanao ya Valentines Day 2018 ambapo zari Hassan aliingia katika mtandaoi wake wa Instagram ambapo ana wafuasi milioni 5.4 ili kutangaza kwamba alikuwa anasitisha uhusiano wake wa miaka 3 na nyota huyo wa wimbo wa 'tetema'.
Zari Hassan alilaumu uzinzi na ukosefu wa heshima kama kitu kilichomshinikiza kujitenga na Diamond.
Hata hivyo Diamond aliamua kuendelea na maisha yake na mtangazaji wa Kenya tanasha Oketch ambaye ameapa kufunga ndoa naye.
Zari Hassan ana watoto wawili na Diamond na wengine watatu na mumewe wa zamani marehemu Ivan Ssemwanga.
Tayari kuna habari kwamba Diamond na Tanasha wameanza maandalikzi ya harusi yao kimya kimya.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...