Thursday, April 18, 2019

RC Mara atoa agizo katika halmashauri kuhusu zao la kahawa


Na Timothy Itembe, Mara

Mkuu wa mkoa Mara,Adamu Kigoma Malima amezitaka halmashauri zake 05 zinazojishugulisha na kilimo cha  zao la kahawa kuhakikisha kilimo hicho kinapanda kutoka Tani 2000 hadi kufika Tani 3200 kwa mwaka ifikapo mwaka 2022.

Malima aliongeza kuwa mkakati mwingine wa mkoa Mara katika zao la kahawa ni kuhakikisha kuwa Mara chini ya mwavuli wa wenyeji wake wilaya  Tarime wanalima Kahawa kwa wingi na  yenye Ubora ili kuwavutia wanunuzi na kuongeza kipato.

"Tunahitaji kilimo cha kisasa chenye tija ili kuongeza wingi na ubora  wa Kahawa kwa hali hiyo tunatarajia kuwa na soko la kahawa hapa hapa Tarime badala ya kusumbuka kwenda kutafuta Masoko nje ya Tarime kwa hali hiyo tutakuwa tumepunguza garama za usafirishaji ambazo zinatutesa huku tukipata fedha kidogo ya kuendeshea shuguli za maendeleo ikiwemo ya kifamilia"alisema Malima.


Malima alitumia nafasi hiyo kuzitaka halimashauri hizo ambazo ni Tarime,Butiama,Bunda,Serengeti na Rorya chini ya mwavuli wa wenyeji wao wilaya Tarime kuandika andiko la kuomba mkopo wa fedha ifikapo Aprili 30  kutoka ndani ya  Benki ya TADB ili kuongeza jitihada za kilimo cha kahawa kutoka tani zilizopo hadi kufikia malengo waliojiwekea ndani ya miaka 05.

Kwa upande wake moja wa Bodi ya kahawa,Melkiad Masawe alisema kuwa kazi ya bodi ni kutafuta masoko na kuwa ili wakulima waweze kunufaika na kilimo cha kahawa ni sharti walime kwa kuzingatia kanuni za kilimo pamoja na wakulima kujiandikisha katika Daftari la kilimo hai.

Masawe aliongeza kuwa changamoto wanayo kumbana nayo nipamoja na Bei ya kahawa kushuka sokoni na kusababisha wakulima kukata tama katika kilimo cha kahawa kiasi kwamba fedha wanayopata haikidhi mahiyaji.

Mwenyeji wa kikao hicho cha wadau wa zao la  wakahawa  ambacho kilifanyikia Nyamwaga wilayani Tarime ili kujadili mkakati wa kufikia lengo la Tani 5000 ifikapo mwaka 2022,Afisa kilimo na Umwagiliaji wilaya Tarime,Sluvanus Gwiboha alisema kuwa kuhakikisha kuwa lengo linafikiwa sharti wakulima wapande kahawa ya Vikonyo.

Mkakati uliopo kwa halmashauri ya Tarime ni kuzalisha kahawa kwanjia ya vikonyo na Mbegu ili kuongeza uzalishaji kwa eneo kutoka tani 0.8 hadi tani 1.5 kwa heka,kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 2000 hadi tani 3200 kwa mwaka,kuandaa vitalu vitatu vitakavyozalisha miche 1,005,000 ifikapo 2021/2022.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...