Monday, April 22, 2019

Interpol kutuma kikosi cha uchunguzi Sri Lanka

Polisi ya kimataifa Interpol inapeleka timu ya wachunguzi ikiwa ni pamoja na wataalamu wa kuwatambua wahanga wa majanga nchini Sri Lanka kusaidia mamlaka nchini humo baada ya mashambulizi mabaya ya mabomu ya kujitoa muhanga jana Jumapili yaliyosababisha vifo vya takriban watu 300.

Interpol imesema inapeleka timu hiyo ya wataalamu wa uchunguzi wa maeneo palipofanyika uhalifu kufuatia ombi kutoka serikali zya Sri Lanka.

Wataalamu waliopelekwa ni wabobezi pia katika kung'amua vilipuzi, kukabiliana na ugaidi na utambuzi wa wahanga. Katibu mkuu wa Interpol Juergen Stock amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa msaada wowote utakaohitajika.

Sri Lanka ilisema mapema leo kwamba inahisi kundi la itikadi kali la National Thowheeth Jama'ath limehusika na mashambulizi hayo na kuahidi kuomba usaidizi wa kimataifa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...