Watu wanaoishi katika mji mkuu wa Msumbiji Maputo wameonywa kutokea kwa hali mbaya zaidi kutokana na kimbunga kikali. Tufani iliyopewa jina la Idai, ambayo inabeba upepo wenye kasi ya kilomita 225 kwa saa itasababisha kimbunga kikali karibu na bandari ya Beira, mji wenye watu wapatao laki tano.
Kwa mujibu wa BBC. Mvua kubwa iliyonyesha nchini humo tayari imesababisha vifo vya watu 100 nchini Msumbiji na Malawi. Beira ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Msumbiji ambapo bandari yake iko katika mdomo wa mto Pungwe ambao umekwenda mpaka Zimbabwe.
Kitengo cha hali ya hewa cha Ufaransa ambacho kinashughulikia maeneo yanayodhibitiwa na Ufaransa katika eneo la Bahari ya Hindi kimeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya kutokana na maji kujaa mengi.
Baadhi ya picha zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha madhara katika mji huo wa Beira wakati kimbunga hicho kikikaribia kwa miti mingi kuanza kung'oka.
Msumbiji imekumbwa na vimbunga vingi katika siku za nyuma ikiwemo kimbunga Eline mwaka 2000 kilichoua watu 350 na wengine 650,000 kuyakimbia makazi yao. Na mji wa Beira ndio mara kwa mara unakumbwa na hali hiyo.
Msumbiji ni nchi ambayo iko katika hatari ya kuathiriwa zaidi barani Afrika pale hali mbaya ya hewa inapotokea
Source
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...