Saturday, March 23, 2019

Jamii yahimizwa mshikamano na kuheshimu mamlaka



Na.Ahmad Mmow,Nachingwea.

Jamii nchini imehimizwa kuendeleza mshikamano na kuheshimu mamlaka ili kudumisha amani na kuepuka migogoro.

Wito huo umetolewa leo mjini Nachingwea na mwenyekiti wa jumuia ya vijana wa  Ahmadiyya kanda ya Kusini,Abdulaziz Msesemele wakati wa maadhimisho ya kuanzishwa jumuia hiyo duniani.

Msesemele aliyetoa wito huo baada ya zoezi la kuchangia damu salama ilyotolewa na baadhi ya waumini wa dhehebu la Ahmadiyya katika hospitali ya wilaya ya Nachingewa,alisema jamii inchini inawajibu wa kudumisha amani,kutii na kuheshimu mamlaka ili kuepuka migogoro inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

 Alisema uislamu unahimiza kumtii Mwenyezi Mungu,mtume Muhammad S.A.W na na wenye mamlaka.Hivyo jamii ya kiislamu na isiyo ya kiislamu inawajibu mkubwa wa kuzingatia hayo ili kudumisha amani na ustawi wa nchi na dunia.

"Tunaposema wenye mamlaka sio viongozi wa dini tu.Bali wenye mamlaka hata ya utawala na uongozi ambao wamechaguliwa au kuteuliwa na jamii husika," alifafanua Msesemele.


Aidha kiongozi huyo wa jumuia ya vijana kanda ya Kusini alisema kwakutambua umuhimu wa elimu,wamejipanga kujenga shule za chekechekea hadi sekondari katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuangalia mahitaji ya jamii ya maeneo husika.

"Tupo kwenye mpango wa kujenga shule za chekechea,msingi na sekondari.Bali mpango huo tutatekeleza kwa awamu kutegemea uwezo wetu," alisisitiza Msesemele.

Maadhimisho ya kuanzishwa jumuia hiyo na siku ya masihi aliyehaidiwa,Mirza Ghullam Ahmad ufanyika kila mwaka duniani pote.Ambapo kwa kanda ya Kusini yameadhimishwa mjini Nachingwea.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...