Tuesday, February 12, 2019

Dkt. Mwigulu Nchemba: Tundu Lissu Aliposhambuliwa, Rais Magufuli Alinipigia Simu


Mahojiano ya Mbunge wa Iramba, Dkt. Mwigulu Nchemba kupitia Kipindi cha Clouds 360 pale Clouds Tv kwa ufupi..

Maswali muhimu aliyoulizwa:

Kwanini tangu utenguliwe uwaziri wa Mambo ya Ndani na Rais Dkt. John Magufuli, umekuwa kimya sana?

"Unajua ukiwa kwenye nafasi ya uwaziri vipo vitu vingi vya kuvisemea (mambo mbalimbali yanayotokea nchini). Ndio maana sasa hivi nipo kimya. Nimebaki na vitu viwili tu vya kusemea; mambo ya jimboni kwangu na kazi nzuri inayofanywa na serikali yangu"

Kuna tofauti gani ya Uwaziri na Ubunge?

Hakuna tofauti na maisha yangu hayajabadilika. Nilipokuwa waziri kwenye msafara wangu sikutaka magari yasimamishwe ili nipite. Kwa sababu nilikuwa nafahamu kuna wengine walikuwa wanawahi ndege "airport', wengine wagonjwa na wengine makazini sikutaka kuwachelewesha. Nilikuwa mtu wa kawaida (Mtu wa Watu), ndio maana sioni tofauti na sasa nilivyobaki na ubunge pekee".

Rais Magufuli alivyokutumbua Ulijisikiaje? Ulikasirika?

"Nilisema nilipokuwa kwenye mkutano jimboni kwangu Iramba, nilimshukuru sana Rais wangu John Magufuli kwa kunipa nafasi hiyo ya uwaziri. Sisi ni wafugaji, siku baba akikwambia usiende kuchunga utakasirika? Huwezi".

Vipi kuhusu kugombea urais 2020?

"Kwa kazi nzuri anazofanya Rais wetu John Magufuli, kila mwanaCCM anajua na kufahamu. Kwa sasa nipo bize na jimbo langu, sina mpango wa kugombea URAIS".

Ishu ya "Askari'' aliyemtolea Nape bastola.

"Sikuwahi kusema sio askari. Nilisema sio Polisi. Nilimwelekeza IGP kuchukua hatua aliniambia yule jamaa sio polisi. Kuna utaratibu wa kuchukua hatua na sio kila hatua inatangazwa kwenye vyombo vya habari"

Wana-Singida wakikuuliza Tundu Lissu yuko wapi huwa unawajibu nini? 

"Wanasingida wote wanajua kilichotokea na wanazo taarifa za maendeleo yake. Wanajua alipo. Tatizo lililopo ni ukinzani wa taarifa zinazosambazwa na kunyoosheana vidole hasa na chama chake. Mfano kwenye uchaguzi mdogo walikuwa wanasema msiwape kura hawa wamempiga mwenzetu. Jambo ambalo sio sawa.

"Tundu Lissu aliposhambuliwa, Rais Magufuli alinipigia simu akanipa maelekezo kuchukua hatua haraka sana na wahalifu wakamatwe haraka sana''

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...