Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameungana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi, familia, ndugu, jamaa na marafiki kuupokea mwili wa mmoja wa waanzilishi wa makampuni ya IPP Mama Mercy Anna Mengi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mwili huo umewasili leo majira ya Saa 4 asubuhi katika uwanja wa ndege wa KIA ukitokea jijini Dar es salaam na kupelekwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Shanty Town ambako ibada fupi yakuombea mwili wa marehemu ilifanyika na kuongozwa na Mchungaji Meena wa Kanisa la KKKT Usharika wa Moshi Mjini.
Mchungaji Meena amesema ndugu na marafiki wanapotafakari safari ya mwisho ya Mama Mercy Anna Mengi watambue njia hiyo aliyopita kila mtu atapita hivyo jambo kubwa ni kuimarika katika imani na kuendelea kuishi katika maisha ya ushuhuda na kusaidia wengine bila kuogopa wala hofu kwakuwa Mungu atazidi kuwaimarisha.
Mwili wa mama Mercy Anna Mengi unatarajiwa kuagwa kwa mara ya mwisho hapo kesho baada ya ibada itakayofanyika katika Kanisa la KKKT usharika wa Moshi Mjini na kisha kupelekwa kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele katika mahala palipotengwa na wanafamilia.
Source
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
