Friday, November 16, 2018

Mtoto Aokotwa Akiwa Amefariki Katika Mtaa wa Sido Mkoani Njombe


Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 2-3 ambaye hajajulikana jina lake amekutwa ametupwa korongoni karibu na Msitu uliopo pembezoni mwa kanisa la EAGT

Mtendaji wa Mtaa, Rehema Ngailo amesema alipata taarifa ya kuonekana kwa mwili huo mapema asubuhi ya leo na kuijulisha Polisi

Amesema "Tumesambaza taarifa kwa Wananchi kuangalia kila nyumba kama kuna mtu aliyekuwa na mtoto na sasa hana ili tupeane taarifa na kumtambua aliyehusika"

Wiki mbili zilizopita mtoto mwingine mchanga aliokotwa katika dampo la Kipagamo mjini Makambako akiwa hai na kupelekwa kituo cha kulelea watoto cha Tumaini Ilunda
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...