Friday, November 16, 2018

MOSHI WATOA VIFURUSHI VYA MAJENEZA


Kama ulidhani vifurushi vya muda wa maongezi na data vinatolewa na kampuni za simu za mkononi pekee, utakuwa unakosea; sasa kuna vifurushi vya majeneza.

Tena si tu vifurushi, bali sasa huduma ya mazishi, kaburi na shughuli nyingine za kuwalaza ndugu waliofariki katika nyumba zao za milele, zimerahisishwa.

Mteja akinunua jeneza mapema kabla ya kifo chake, ana uhakika wa kupata punguzo la bei la hadi asilimia 30, lakini pia atakuwa na uhakika wa huduma nyingine za matengenezo ya kaburi kama atakubaliana na watoa huduma.

"Unajua kila mtu lazima afe na ndiyo maana watu wanaandika wosia," alisema Macmillan Siraki, mkurugenzi wa kampuni ya Godmark Funeral Directors ya mjini Moshi iliyoanzisha huduma ya vifurushi hivyo vya majeneza.

"Unapanga vitu vyako ukiwa hai. Ukishakufa watu watakupangia. Hawatapanga kama wewe unavyotaka

"Hata jeneza, hakuna atakayekununulia kama ulivyotaka wewe wakati ukiwa hai. Kuna baadhi ya watu hawathamini mtu akishakufa na pengine hata fedha ya jeneza ni ya kwake.

Alisema walipoanzisha huduma hiyo ya punguzo, watu wengi walijitokeza.

"Wapo walioonyesha interest (nia) na baadhi wameshatoa oda. Lakini makubaliano yetu ni kutunza siri hii hawataki iwe public (hadharani)," alisema Siraki.

"Walikuwa wanauliza tu maswali kama miundo inapobadilika inakuwaje lakini tumekubaliana kama ikitoka design (muundo) mpya akiwa hai, tutambadilishia labda kama atataka la gharama zaidi.

"Mara nyingi hatuongezi fedha. Kama mtu amekuachia fedha yake maana yake na wewe umeitumia kuzungusha kwenye biashara. Huna sababu ya kuongeza bei zaidi ya kumpa design nzuri iliyotokea."
Via Mwananchi

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...