Baada ya tetesi kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima yupo mbioni kujiunga na matajiri Azam FC, Hatimaye tetesi hizo zimeibua vita ya maneno kati ya Msemaji wa Simba, Haji Manara na Mchambuzi wa Soka wa kituo cha redio cha Clouds FM, Shaffih Dauda.
Shaffih Dauda kupitia ukurasa wake wa Instagram aliposti picha ya Niyonzima akiwa amevaa jezi moja iliyowekwa rangi ya Simba na Azam FC na kisha kuiandikia maneno yaliyosomeka "Kwani kuna habari gani?"
Baada ya hapo, Haji Manara aliona sio kesi akaamua kumjibu Shaffih kwa kuandika ujumbe mzito huku akimshambulia mchambuzi huyo kuwa anatumika na ni adui mkubwa wa Simba.
"Tunajua Shaffih unatumika na Maadui wa Simba kutaka kutuvuruga kusudi ili kubalance na cc tuonekane tuna mgogoro na wachezaji wetu!!. Hatuna Niyonzima yupo camp now na leo atacheza ikimpendeza kocha dhidhi ya Bata Bullets, Hivi mtu muungwana kabisa unawezaje kuandika uongo na kufikia kumvalisha jezi ya team nyingine mchezaji aliye na mkataba na klabu yetu kama c uchochezi na uhuni wa kishamba?,"ameandika Haji Manara.
Akiendelea kutupa madogo kwa Shaffih Dauda, Manara amesema kuwa mtangazaji huyo kuna kipindi aliomba kazi Wasafi TV na alichomolewa nje.
"Mimi najua uliomba ajira pale @wasafitv na wakakutalia mbona hatujapost umevaa T-shirt ya @diamondplatnumz
Unatutafuta ugomvi wa kusudi na mabosi zako tunaowaheshimu sana ila soon Simba itafanya maamuzi makubwa juu yako na Juu ya radio na TV unayoifanya kazi
Au kwa kuwa washabiki wa Yanga walitaka kukupiga ndio maana huandiki habari zao za wachezaji kudai Mishahara ya wachezaji? Simba haina ujinga wa kupiga Waandishi ila tunazo njia sahihi za kukunyoosha…Mara kadhaa umekuwa unaandika upuuzi against us tunakuvumilia tu,sasa sitakuacha,"amemaliza Manara.
Manara na Shaffih Dauda wamekuwa wakiingia kwenye majibizano mazito mara kwa mara, na hii inasemekana ni kutokana na mtangazaji huyo kipindi cha nyuma alishawahi kuomba nafasi ya usemaji wa klabu hiyo.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...