Friday, August 3, 2018

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YASHIRIKI MAONESHO YA KILIMO NA SHEREHE ZA WAKULIMA (NANE NANE) MKOANI SIMIYU

Ili kuhakikisha kila Mwananchi anapata huduma bora za matibabu ya moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatoa huduma ya upimaji wa magonjwa hayo katika maonyesho ya Kilimo na Sherehe za wakulima (nanenane) yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. Maonyesho hayo yanafanyika katika uwanja wa Nyakabindi uliopo Halmashauri ya mji wa Bariadi.

Huduma zinazotolewa na Taasisi yetu ni upimaji wa vihatarishi vya magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, elimu ya lishe bora, kuelezea kwa kina huduma zinazotolewa na Taasisi, kutoa Rufaa ya moja kwa moja kwa wananchi watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitaji kupewa rufaa.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iko kwa ajili ya kutoa huduma bora na kutoa elimu inayohusiana na magonjwa ya Moyo kwa wananchi. Wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu pamoja na mikoa ya jirani mnakaribisha kutembelea Banda letu ili muweze kupata huduma zetu. Karibuni sana.

"Afya ya Moyo wako inatuhusu"

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...