Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mabingwa wa Soka ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Wekundu wa Msimbazi, Simba wamesema sasa wanaanza kuuza jezi zao halisi 'Original' ili kuongeza mapato ya klabu.
Hayo yamesemwa yamebainishwa jana Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah (Try Again) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu yanayojiri kuelekea siku Muhimu kwa timu hiyo ambayo maarufu kama Simba Day.
Abdallah amesema kuwa katika Simba Day ya Mwaka huu klabu hiyo imebadilisha mfumo wa upatikanaji wa jezi kwa wanasimba kuvaa, kila mtu jezi yake ambayo aileti manufaa katika klabu matokeo yake sasa kila mtu ataweza kupata jezi hizo siku ya Simba Day kwa Mawakala Maalum watakaopitishwa na bodi ya Simba.
"Tumeandaa mzigo wa kutosha wa jezi kwa ajili ya wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba hivyo tunawaomba wafike uwanjani siku ya Tarehe nane ambayo Simba Day,kuja kushuhudia wachezaji wapya wakitambulishwa na burudani nyingi ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya wanasimba" Amesema Abdalah
Ametaja kuwa mbali na jezi hizo kupatikana uwanjani hapo siku ya mechi pia klabu hiyo itafungua Duka kubwa litakalokuwa linauza Vifaa vya Simba pale Msimbazi Kariakoo hivyo kila mtu atakayekosa jezi uwanjani anaombwa kupata fursa ya kwenda kununua katika makao makuu ya timu hiyo.Abdalah ametoa wito kwa wapenzi wa Klabu ya Simba kuacha kununua jezi ambazo sio Original kwani kwa kufanya hivyo awawezi kusaidia kukuza uchumi w atimu yao.
Source