STAR Media (T) Ltd, imewaomba radhi wateja wake pendwa na umma kwa ujumla kwa kutopata chaneli za bure kwa muda sasa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji Star Media(T)Wang Xiaobo amesema leo kuwa hiyo imesababishwa na kukosekana kwa elimu na mawasiliano mazuri kuhusu aina ya tofauti za dikoda (ving'amuzi) tulizonazo, ambayo yamesababisha kwa wateja wao kuendelea kulipia chaneli za bure.
"Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa ziko aina mbili za dikoda, ya kwanza ni ile ya Chaneli za bure (FTA) ambayo mteja halazimiki kila mwezi ili kutazama chaneli za bure.
"Na nyingine ni ya chaneli za kulipia, ambayo mteja atatakiwa kulipia kifurushi chake kila mwezi," amesema
Ameongeza kwa wateja wapya, dikoda (ving'amuzi) hizo zinapatikana kwenye maduka yao pamoja na mawakala wao, lakini kwa wateja ambao tayari wameshanunua dikoda (ving'amuzi) za kulipia wanaweza kubadilisha dikoda (ving'amuzi) zao kuwa FTA kwa kutembelea katika ofisi zetu na kupata utaratibu.
Amesisitiza Star Media (T) Ltd, itaendelea kuzingatia masharti yote ya leseni, pia inaufahamisha umma kwamba imekubali kufuata na kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwamo kulipa faini ambayo tayari imeshaanza.
Pia wanawafahamisha umma wa watanzania kwamba sasa wanaweza kuendelea kufurahia chaneli za bure na huduma zetu kwa ujumla.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Ninakualika kutazama Video Mpya kabisa mwaka 2021 kutoka kwa Msanii Yobat amemshirikisha Bhudagala Ng'wana Malonja na Shija Kadoke wim...
