Msanii wa filamu bongo, Daudi Michael maarufu kama 'Duma' amedai wasanii wengi wameshindwa kuendelea kuishi katika soko la filamu nchini kutokana na kuzoea kupewa fedha na baadhi ya wasambaji ili kusudi waweze kufanya kazi waliotumwa jambo ambalo kwa sasa watu hao hawafanyi tena.
Duma amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii kupungua katika soko la filamu, jambo ambalo wafuatiliaji na wapenzi wa tasnia hiyo kudai huenda bongo movie imekufa au kutolipa katika nyakati hizi.
"Ninapambana na nitaendelea kufanya hivyo hadi tone langu la mwisho, ili kusudi soko la filamu liweze kurudi kwenye 'chart' yake kama ilivyokuwa hapo awali. Sitoweza kukubali kushindwa katika hili", amesema Duma.
Mbali na hilo, Duma amefafanua baadhi ya mambo kuwa kinachowafanya wasanii wengi wa filamu kushindwa kutoa kazi zao kama ilivyokuwa hapo awali ni kutokana na ma-boss waliokuwa wanawapa fedha, sasa hawatoi tena.
"Ma-boss hawatoi fedha tena sasa hivi kutokana kutosheka na movie walizokuwa nazo, wasanii waliowengi hawamiliki filamu za kwao binafsi bali wao wanakuwa kama vibarua tu wa kufanyakazi kutokana na bajeti walizopewa na watu hao", amesisitiza Duma.
Kwa upande mwingine, Duma anatarajia kuachia kazi yake mpya kesho inayokwenda kwa jina la 'nipe changu', ambayo imejumuisha wasanii mbalimbali pamoja na kuwa na maudhui ya kitofauti na jinsi watanzania walivyozoea kuzitazama.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
