Friday, August 3, 2018

JWTZ yatangaza nafasi za madaktari wa Binadamu

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kuwa linauhitaji mkubwa madaktari katika taaluma mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza nafasi za ajira katika jeshi hilo, Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano na Msemaji wa Jeshi la JWTZ Kanali Ramadhan Dogoli amesema kuwa watanzania wenye sifa kuomba nafasi katika jeshi hilo .

Amesema nafasi za madaktari wa binadamu zinatolewa ili kuongeza idadi ya watalaam wa Tiba watakaotoa huduma za afya katika hospitali za jeshi, Vituo vya Afya na Zahanati kulingana na mahitaji ya sasa na siku zijazo.

Nafasi zinazohitajika ni Doctor of Medicine, Doctor of Dental Surgery, Bachelor of Pharmacy, BSC Health System Management, Bachelor in Labaratory Science, Bachelor of Science in Nursing, Bachelor of Science in Physiotherapy pamoja na bachelor of Science in Prosthetics and Orthotics.

Kanali Dogoli amesema kuwa sifa kati ya umri wa miaka 18-28, muombaji awe hajawahi kupatikana na hatia za kijinai mahakamani na kufungwa jela, kuhitimu pamoja na mafunzo ya vitendo na kutunikiwa vyeti na kusajiliwa na Bodi.

Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na jeshi hilo wafike katika kambi ya Jenarali Abdallah Twalipo Mgulani Agasti 28 kuanzia 1:00.
Waombaji watajigharamia Chakula, Usafiri

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...