Tuesday, March 4, 2025

Rais Samia apongezwa kwa kutoa sadaka ya iftari kwa wahitaji Tanga


Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Abubakary Zuberi Bin Ally amewataka waumini wote wa dini ya kiislam nchini kuitunza neema waliopewa na Mungu  hususani kipindi huki cha Mfungo wa Ramadhani .

Hayo aliyasema wakati akizungumza katika msikiti wa Tamta uliopo jijini Tanga ambapo walifuturisha watu mbalimbali  wakiwemo watoto yatima  na wenye uhitaji kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samaia Suluhu Hassan.

Aidha alisema kuwa ni vyemq waumuini kuitunza neema waliojaaliwa na Mungu  kwani neema ya Mungu ndio inayowalinda katika maisha yao, sambamba hayo alimshukuru Rais Samia kwa kuwashirikisha viongozi wa dini katika ziara yake ya siku saba katika mkoa wa Tanga.

Kwa Upande wake Mwenyeiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu  Abdulrahaman Abdalah alisema wanamshukuru na kumpongeza Rais Samaia Siluhu Hassan  kwa kuvunja rekodi ya kukaa kwa siku siku saba katika mkoa wa Tanga kwani haijawahi kutokea.

Naye Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewaponeza na kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Tanga kwa mapokezi mazuri ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Samaia Siluhu Hassan Tangu alipoanza ziara Yake ya Kikazi  mkoani humo ambapo alitembelea wilaya  zote   ndani ya mkoa.
 
Alisema kwa namna ambayo wananchi waliitokeza kwa wengi serikali imefarijika sana na tunawaahidi kuendelea kushikamana siku zote kwani wameishimisa serikali  mkoa jambo ambalo limedhihirisha Upendo kwa Mh.Rais Dkt Samia.
 
Balozi Buriani alisema kuwa ujio wa Rais Dkt. Samia kwa mkoa Tanga  umeleta hamasa  kubwa kwani amezindua miradi mingi iliyogharimu kiasi cha sh.Tirilion moja na Milioni Mia nane  jambo ambalo imeonyesha kuwa kazi kubwa iliyofanywa na serikali  .

"Tumshukuru sana rais kwa kutuzinduliwa miradi mikubwa ikiwemo  Bandari  uliogharimu Bilion 429 ,jengo la utawala Bumbuli wilayani Lushoto,Hospitali ya wilaya ya Handeni ,Mradi wa maji wa miji 28 na miradi mingine mingi ." alisema Balozi Buriani


    

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...