Kiungo wa Yanga SC, Paccome Zouzoua Peodoh, ameomba kuondoka klabuni hapo baada ya kupokea ofa kutoka miamba wa Misri, Al Ahly.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, Zouzoua amewataka mabosi wa Yanga kuamua haraka kama wanataka kuuza sasa au wamuache aondoke bure mwishoni mwa msimu, kwani hana mpango wa kuongeza mkataba mpya.
Pia, kuna uwezekano mkubwa wa kiungo huyo kukosa mechi ya kesho, jambo ambalo linaweza kuathiri mipango ya kocha wa Yanga.
Je, Yanga SC itamruhusu kuondoka au itapambana kumbakiza kikosini?
Endelea kufuatilia Diva Media Africa kwa taarifa zaidi!
Source