Thursday, August 5, 2021

Jack Grealish kuweka rekodi ya usajili EPL



Kiungo wa kimataifa wa England Jack Grealish atafanya vipimo vya afya leo Alhamisi ikiwa katika harakati za kukamilisha usajili wake wa wakujiunga na Manchester City akitokea Astoni Villa. Kwa mujibu wa ripoti kiungo huyo atasaini mkataba wa miaka 5.
Ijumaa ya wiki iliyopita Manchester City walipeleka ofa ya pauni milioni 100 zaidi ya billion 322 kwa pesa za kitanzani katika klabu ya Aston Villa kama ada ya uhamisho ya Grealish, ambapo kiwango hicho cha pesa ndicho kilikuwa kwenye mkataba wa mchezaji huyo na Villa kama kuna timu inataka kuvunja mkataba wa mchezo huyo basi ilikuwa lazima ilipe dau hilo na Man City wamefanya hivyo.

Usajili huu ukikamilika utakuwa ndio usajli wenye thamani kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika historia ya soka la England, kwa sasa rekodi ya usajili wenye thamani zaidi ni ule wa Paul Pogba ambaye alinunuliwa na Manchester United kutoka Juventus ya Italia mwaka 2016 kwa ada ya Pauni million 93 taklibani billion 300 za kitanznaia.

Jack Grealish mwenye umri wa miaka 25 ni mchezaji aliyekulia kwenye misingi ya Aston Villa, alijiunga na klabu hiyo katika timu ya vijana mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 6, na ameshaitumikia Villa kwenye misimu 10 ya mashindano. Msimu uliopita alicheza michezo 27 na alifunga mabao 7 na akitoa pasi za usaidizi wa mabao (assists) 10.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...