Wednesday, July 14, 2021

Watu 17 waokolewa kutoka mikononi mwa Boko Haram


Watu 17 waliotekwa nyara na shirika la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria waliokolewa.

Msemaji wa Jeshi Onyema Nwachukwu, alitangaza kuwa jaribio la shambulizi la Boko Haram lilizuiliwa katika kijiji cha Auno kilichoko jimbo la Borno.

Nwachukwu alisema kuwa baada ya shambulizi lililokuwa limezuiliwa, watu 17 waliokolewa katika operesheni ya jeshi dhidi ya Boko Haram kwenye barabara kuu ya Maiduguri-Damaturu.

Akibainisha kuwa mateka hao walikuwa na afya njema, Nwachukwu alieleza kwamba watu hao waliwasilishwa kwa serikali ya jimbo la Borno.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...