Monday, July 5, 2021

Tabia Tano (5) Za Muhimu Kwa Mjasiriamali Mwenye Mafanikio


Kwa kawaida siri ya mafanikio makubwa  kwa mjasiriamali yeyote yule ipo kwenye tabia zake. Tabia hizi ndizo ambazo zinazomtofautisha mjasiriamali mwenye mafanikio na yule ambaye ana mafanikio ya kusuasua au hana kabisa mafanikio.

Hivyo kwa mantiki hiyo,  ni muhimu sana kwa mjasirimali mwenye mafanikio makubwa  kujijengea  tabia bora zitakazo msaidia kuweza kufanikiwa. Moja kati ya tabia hizo ambazo mjariamali anatakiwa kuwa nazo ili kufanikiwa ni kama hizi zifuatazo:-

1. Kuamka asubuhi na mapema.
Wengi kati ya watu wenye mafanikio makubwa wamefanikiwa sana kujenga tabia hii ya kuamka asubuhi na mapema. Huu ni muda ambao huwasaidia sana kutekeleza majukumu yao ya muhimu mapema zaidi wakati watu wengi bado wakiwa wamelala.

Soma; Mambo Sita (6) Ambayo Mjasiriamali Anatakiwa Kuyafanya Kila Siku.
Wanafanya hivyo kwa sababu, hiki ni kipindi ambacho kinakuwa kimetulia na wala kuna kuwa hakuna makelele ya hapa na pale. Mara nyingi muda ambao watu wenye mafanikio hupenda sana kuamka ni kati ya saa kumi kamili hadi saa kumi na moja kamili asubuhi.

2. Mahusiano na wengine (Networking).
Kati ya kitu muhimu katika safari ya mafanikio ni mahusiano bora na wengine. Kwa kila mjasiriamli mwenye mahusiano bora na watu wengine, inamsaidia sana katika kujipatia fursa mbalimbali ambazo zinajitokeza karibu kila siku.

Ikiwa huna tabia ya kujenga mahusiano mazuri na wengine ni ngumu sana kufanikiwa kama mjasirimali. Hiyo iko hivyo kwa sababu utashindwa kushirikishwa mambo mengi ambayo ni fursa kwako. Kwa nini hautashirikishwa? ni kwa sababu huna mahusiano mazuri na watu wengine.

3. Mipango.
Ukifatilia maisha ya watu wenye mafanikio kwa ukaribu, utagundua ni watu wenye mipango. Si watu wa kuishi tu kama bendera fuata upepo, bali ni watu ambao mambo yao wamejiwekea kwa utaratibu na kuhakikisha wanayafanikisha kwa namna yoyote ile.

Hakuna mtu wenye mafanikio makubwa akaishi kiholela bila kuwa na mipango imara. Jaribu leo kujiwekea mipngo imara juu ya maisha yako, hiyo itakusaidia sana kuweza kufika mbali kimafanikio baada ya muda fulani na utatimiza malengo yako.

4. Kusikiliza.
Mbali na kuamka asubuhi na mapema, kuwa na mahusiano mazuri na wengine na kujiwekea mipango, pia watu wenye mafanikio wana tabia moja muhimu ya kusikiliza. Hawa ni watu ambao huwa si waongeaji muda wote bali pia husikiliza sana ili kujifunza.

Kusikiliza ni moja ya tabia muhimu sana inayowajengea mafanikio. Mengi sana hujifunza kupitia kusikiliza kuliko kuongeongea tu jambo ambalo lingepelekea kujua yale tu peke yake wanayoyajua. Hata wewe kama unataka kufanikiwa ni muhimu sana kujijengea tabia hii ya kusikiliza.

Kwa mjasiriamali yeyote mwenye mafanikio, huzingatia sana tabia hizo ambazo kwa sehemu kubwa humsaidia kumfikisha kwenye kilele cha mafanikio.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...