Wednesday, July 28, 2021

Shaffih Dauda Amchana Manara Vibaya "Nje ya Simba Manara ni Muoga na Mjanja Mjanja"




Binafsi sio muumini sana wa Seasons wala movies za part One mpaka Three, by nature nina uvivu wa kusoma sana au kukaa kwenye mada moja kwa muda mrefu, kutokana na changamoto ya muda

By the way niliwapa aina mbili za Haji Manara, nikawaelezea na wenye kuelewa basi wameelewa, Haji ukishamtoa kwenye kivuli cha Simba na kumuanika yeye peke yake ni muoga na Mjanja Mjanja

Unaweza kudanganya watu ila watu huwezi kuwadanganya kwa wakati wote, moja kati ya vitu anavyoamini ni kuwa Simba ipo ilipo kwa nguvu yake, well and good kwakuwa ni Muajiriwa its fair kuamini hivyo

Ila Simba kufanikiwa kisa maneno yake ni kujidanganya, Simba ilikuwa na mafanikio kabla hata yeye kufika Simba, 1970 huko Simba anacheza Nusu Afrika, 1990 huko Simba anacheza fainali shirikisho, Haji alikuwepo? Ni hoja mfu

Kuendelea kuamini brand ya Simba inalindwa kwa kelele zake huo ni utoto, Simba ina miaka mingi imejitengenezea brand yake na Mashabiki pamoja na wao Viongozi collectively wanaipeleka, kila Mtu akifanya kwa nafasi yake

Brand hailindwi kwa dhihaka wala maneno, brand inalindwa kwa Matokeo uwanjani, vikombe na mipango kazi, mambo yakienda vizuri kila Kiongozi atakachosema basi kinakuwa Lulu, kwa mafanikio ya Simba hata Mwandishi fresh from school akikaa pale ataongea na ataeleweka

Kinachomsumbua Haji ni lifestyle aliyochagua, kama ulipata kazi kwa kelele zako utalazimika kuishikilia nafasi kwa kelele, kama ulipata nafasi kwa Merit basi utaishikilia nafasi yako kwa Merit, hiyo ndio kanuni ya maisha, Haji ni muhanga wa lifestyle yake

Ila kwa kadri Simba inavyopiga hatua itaendelea kubadilika, kuna Uswahili umeachwa na haupo tena Simba, kuliwahi kuwa na makomandoo sasa hawapo tena, kulikuwahi kuwa na wapiga dili na sasa hawapo tena, itafika muda hawatohitaji kelele za Manara, believe me muda utafika

Tunaposema anakosea anakimbilia huruma ya Mashabiki ila endeleeni kumkubusha msiache, Simba atakapofikia level za Al Ahly, Sundowns basi ni eidha yeye abadilike au system imbadili, nadhani ni kanuni ya Maisha

Haji is a prisoner of his own history, nafikiri niifunge hii issue tunamfundis
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...