Tuesday, July 13, 2021

Ndege ya Uganda Yaishiwa Mafuta Dar




ABIRIA wanaokwenda Uganda kwa kutumia ndege ya Shirika la Uganda Airlines walichelewa kuondoka jana jioni katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini, Dar es Salaam nchini Tanzania kwa saa kadhaa baada ya kuishiwa mafuta.
 

Ndege hiyo ilieleza sababu ya kuchelewesha safari yake ni kutokana na kuchelewa kupokea mafuta ambayo walikuwa wameyaagiza.

 

Aidha uongozi wa kampuni hiyo ya ndege iliandika taarifa katika mitandao ya kijamii kuomba radhi kwa tukio lililotokea na kuhaidi tukio hilo kutojirudia siku zijazo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...