Monday, July 19, 2021

Milioni 62 zahitajika kuboresha Machinga Complex - RC Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea Soko la Kariakoo, Kisutu na Machinga Complex walipohamishiwa Wahanga wa Moto Soko la Kariakoo kwa lengo la kujionea Kama Kuna Changamoto ili Serikali iweze kuzitatua na Wafanyabiashara wafanye biashara zao bila usumbufu.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amefurahi kuona wengi wao wamepata Maeneo ya kufanya biashara na wanaendelea na biashara zao Kama kawaida.


Kuhusu suala la wateja, RC Makalla ameahidi kuwa Mstari wa mbele Katika kuwatafutia wateja huku akisisitiza agizo lake la kutaka wasitozwe Ushuru kwa Muda wa miezi miwili Kama sehemu ya kifuta machozi.

Akiwa soko la Machinga Complex, RC Makalla amepokea changamoto ya kukosekana kwa Paa la kuzuia Jua na Mvua ambapo ameahidi kutafuta kiasi Cha Shilingi Milioni 62 ya Ujenzi wa Paa la Kisasa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji la Ilala kuwaondoa Wafanyabiashara wanaoendesha biashara zao kwenye hifadhi za Barabara na kuwatafutia vizimba ndani ya Masoko hayo.

Kwa upande wao Wafanyabiashara wahanga wa Moto Soko la Kariakoo akiwemo Radhid Mohamed ameishukuru Serikali na Viongozi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mzuri waliowapatia na licha ya changamoto waliyoipata wamempatia RC Makalla  zawadi ya Viungo vya Chakula Kama sehemu ya furaha kwa Mambo mazuri Serikali iliyowafanyia.

 

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...