Thursday, July 15, 2021

Hatari yaongezeka ya vita kupamba moto kaskazini mwa Ethiopia

 


Vita vya Ethiopia katika mkoa wa kaskazini wa Tigray, vinaelekea kupamba moto baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kuashiria kwamba serikali yake imebatilisha hatua ya kusimamisha mapigano. 

Wakati huo huo viongozi wa mkoa jirani wa Amhara nao wamesema wanakusudia kuvishambulia vikosi vya Tigray. 

Kikosi cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF, ambacho kimeyakomboa maeneo karibu yote ya jimbo hilo katika wiki tatu zilizopita kinaazimia kuikomboa sehemu ya magharibi ya jimbo hilo ambalo ni eneo kubwa lenye ardhi ya rutuba linalokaliwa na majeshi ya Amhara. 

Majeshi ya Amhara yaliiteka sehemu hiyo wakati wa mapigano ya miezi minane kati ya majeshi ya serikali kuu ya Ethiopia na majeshi ya jimbo la Tigray.

Msemaji wa serikali ya mkoa wa Amhara ameeleza kuwa viongozi wake wanayaandaa majeshi yao ili kupambana na manajeshi ya jimbo la Tigray.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...