Saturday, July 10, 2021

CCM wamuonya mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe kimemuonya mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Njombe Bi,Rose Mayemba kutokana na matamshi anayoyatoa mitandaoni dhidi ya Rais pamoja na viongozi wa Chama na Serikali


Akizungumza na vyombo vya habari ofini kwanke kwa niaba ya Chama,Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi Erasto Ngole amesema.


"Rose Mayemba mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe amekosa adabu,tunamshangaa kwa matumshi anayoyasema kwenye mitandao dhidi ya viongozi mbali mbali wa Chama na serikali hususani Rais"alisema Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe


Aidha amesema "Chama tunalaani kauli za mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe kwenye mitandao kwa nguvu zote,na tunamuleza kuwa anayemchezea ni Rais wa nchi,ndio mwenye vyombo vyote vya dola na ndiye Amiri jeshi mkuu" Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe


Ameongeza kuwa "Watu wanafanya siasa za kurudisha nyuma,tunaviagiza vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa na TCRA,viwafuatilie wanasiasa wote wenye tabia kama za Rose Mayemba mwenyekiti wa CHADEMA,Njombe kwasababu huwezi ukawa na vyombo halafu watu wanamdhihaki Rais ukakaa kimya" Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe


Amesema mwenyekiti huyo wa Chadema ameonyesha dhiahaka kwa Rais kuto kuwa na uwezo "Rose Mayemba mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe,kwenye mitandao ameonyesha kwamba Rais wa nchi hana uwezo,tunamwambia Rose kuwa Rais wa nchi haangaliwi kwa jinsia na upole wake.Ni lazima uwe na adabu yule ndio mtanzania namba moja"Amesema Erasto Ngole


Vile vile Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimempongeza Rais wa Jamahuri ya muungano wa  Tanzania  Mh,Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha nia thabiti ya kuanza kwa maradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo wilayani Ludewa kwa kuwa wananchi wa mkoa huo wamekuwa wakiusubiri kwa muda mrefu.


"Imekuwa ni dana dana toka awamu ya Kwanza kwamba tunaanzisha mradi wa Liganga,lakini mama amekuja na mkakati na ametoa maelekezo kwa wizara zinazohusika tuanze kuchakata chuma wilayani Ludewa.Tunampongeza Mh,Rais" Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe


Katika mitandao kupitia kurasa zake za kijamii mwenyekiti wa Chadema Rose Mayemba amekuwa akiandika jumba mbali mbali kuhusu ufanyaji kazi wa Chama chake huku vile vile akikosoa utendaji mbovu wa viongozi wa serikali na ujumbe mmojawapo ukiwa.


"Rais Tayari ameanza kujibu mapigo ya wapinzani,madai ya katiba mpya ameyaita CHOKO CHOKO..Hizi ni dalili tosha kwamba uwezo wake wa kuhimili mambo mazito ni mdogo sana.Kuna kila dalili akakosa uvumilivu mapma.Matumizi ya Dola hayakwepeki.Tujiandae"ameandika Rose Mayemba kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo twita na Facebook


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...