Tuesday, July 20, 2021

AUAWA BAADA YA KUMPIGA POLISI 'TRAFIKI' KWA CHUMA CHA KUPONDEA MAWE GEITA


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, akionesha chuma kilichotumika kumjeruhi Askari
**
Kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 20-25 amefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi baada ya kumjeruhi kwenye taya na kidevu Askari wa Usalama Barabarani kwa kumpiga na chuma cha kupondea mawe (Moko), wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi Mtaa wa Mwembeni, barabara ya Katoro Ushirombo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuvamiwa na kujeruhiwa askari wa barabarani namba H1619 John Charles lililopelekea wananchi wenye hasira kali kuingilia kati na kumuua mhusika kwa kipigo.

Aidha, Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi wenye migogoro binafsi na Askari kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zinazostahiki.

CHANZO - EATV
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...