Ubelgiji na Finland zimesajili ushindi katika mechi zao za ufunguzi kwa kundi B katika michuano ya mataifa ya Ulaya ya Euro 2020, inayoendelea katika viwanja mbalimbali vya ulaya. Ubelgiji imeipa Urusi kichapo cha mabao 3-0, huku Finland ikiponyoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Denmark.
Katika mechi ya kundi A Wales imetoka sare ya 1-1 na Switzerland. Romelu Lukaku alisherehekea mabao aliyofunga kwa kukimbilia kwenye kamera ya runinga na kupiga kelele kumtumia ujumbe mchezaji mwenzake wa Inter Milan, Christian Eriksen aliyezirai uwanjani, kwa kumwambia anampenda.
Leo hii Uingereza itashuka dimbani kuchuana na Croatia. Halafu Austria itacheza na Macedonia kaskazini na Uholanzi ikipige na Ukraine.
