Wednesday, June 2, 2021

TAKUKURU Lindi yawafikisha mahakamani wafanyabiashara watatu kwa tuhuma ya kuuza kiwatilifu kisichosajiliwa


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani  Lindi kwakushirikianana ofisi ya mashtaka, leo imewafikisha mahakamani wafanyabiashara watatu kwa tuhuma za kuuza kiwatalifu kisichosajiliwa.

Leo akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Lindi iliyopo katika manispaa ya Lindi, mkuu wa taasisi hiyo wa mkoa wa Lindi, mhandisi Abnery Mganga alisema katika kutekeleza jukumu lake la Kuzuia  na Kupambana na Rushwa ili kuimarisha utawala bora kwa kushirikiana na kikosi kazi toka taasisi ya utafiti wa Dawa za Mimea Tanzania (TPRI) ilibaini kwamba wafanya biashara hao walikuwa wanauza kiwatilifu aina ya SELECRON ambacho hakijasajiliwa.

Mhandisi Mganga alisema tarehe 14/04/2020, ofisi ya TAKUKURU ya mkoa wa Lindi ilipokea taarifa kwa njia ya simu kutoka TPRI ikieleza kwamba baadhi ya wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo katika wilaya za Ruanga na Nachingwea wanauza kiwatilifu hicho ambacho kinazalishwa bila kibali cha TPRI na hakijasajiliwa.

Mganga ambaye aliweka wazi kwamba kiwatilifu hicho kinamadhara kwa binadamu alisema TAKUKURU kwakushirikiana na TPRI tarehe 30/4/2020 ilifanya ukaguzi kwenye maduka ya wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wilayani Nachingwea. Ambapo ilibaini kwamba ni kweli kiwatilifu hicho kilikuwa kinauzwa kwa shilingi 16,000 kwa kila chupa moja yenye ujazo wa mili lita 300.

" Kati ya maduka ya pembejeo yaliyokaguliwa katika wilaya ya Nachingwea ni pamoja na duka la Bwana Abdallah Luyaya ambaye anatumia jina la biashara la LUYAYA KILIMO KWANZA na duka la Bwana Ismail Tebwa ambae anatumia jina la biashara la TEBWA AGRO DEALER. Hao ni kati ya watatu watakaofikishwa mahakamani leo, kwani walibainika wanauza kiwatilifu hicho," alisema mhandisi Mganga.

Mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Lindi aliongeza kusema kwamba tarehe 01/05/2020 kwa mara nyingine na kwa kushirikianana  kikosi kazi kutoka TPRI ilifanya ukaguzi katika wilaya ya Ruangwa ambako miongoni mwa maduka yaliyokaguliwa ni duka la Jasmine Agrovet ambalo mmiliki wake ni Jasmine Mwalami ambae pia nimiongoni mwa waliofikishwa mahamani leo kwa tuhuma ya kuuza kiwatilifu hicho ambacho kinatajwa kinamadhara kwa binadam.

Ofisa huyo wa juu wa TAKUKURU katika mkoa wa Lindi alisema Bwana Abdallah Luyaya na Bwana Ismail Tebwa ambao ni wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wilayani Nachingwea walikutwa na SELECRON 720 EC 500ML ambacho hakina kibali na hakijasajiliwa na Taasisi ya Utafiti wa   Dawa za Mimea. Huku akibainisha kuwa katika duka la Jasmine Agrovet lililopo wilayani Ruangwa lilikutwa likiuza kiwatilifu cha aina hiyo chenye sifa za zilizokutwa kwenye maduka ya Tebwa AGRO DEALER na KILIMO KWANZA.

Alisema baada ya kukamilika ukaguzi, taasisi hiyo ilifanya uchunguzi ili kujua kama wauzaji walikuwa na vibali vya kuuza kiwatilifu hicho na jinsi wanavyoingiza viwatilifu kwenye maduka yao. Ambapo ilibainika kwamba viwatilifu visivyo sajiliwa vinaingizwa kwa siri nahata usafirishwaji wake ni wa siri pia. Ambapo rushwa inatumika kwakiasi kikubwa kurahisisha   uingizaji na usafirishaji huo.

" Pamoja na uchunguzi kujieleza kwenye sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007, pia uchunguzi ulifanyika kwa kuzingatia sheria ya kulinda mimea namba 13 ya mwaka 1997, sura ya 133," alibainisha mhandisi Mganga.

Aidha ofisa uchunguzi kiongozi huyo wa TAKUKURU mkoa wa Lindi aliweka wazi kwamba watuhumiwa wote watatu( Tebwa, Luyaya na Mwalami) leo wamefikishwa mahakamani. Nikutokanana kukamilika uchunguzi baada ya jalala lililopelekwa kwa mkurugenzi wa mashtaka la kuomba kibali cha kuwafikisha mahakamani kufanyiwa kazi na mkurugenzi huyo wa mashtaka.

Kwamujibu wa mhandisi Mganga nikwamba watuhumiwa hao ambao watashitakiwa katika mahakama za wilaya za Nachingwea na Ruangwa watatakiwa kujibu mashitaka ya kuonesha kwa lengo la kuuza kiwatilifu kisicho kuwa na vibali wala kusajiliwa, na kuuza kiwatilifu kisichokuwa na kibali na kisichosajiliwa.

Watuhumiwa Ismail Tebwa na Abdallah Luyaya wameshitakiwa katika mahakama ya wilaya ya Nachingwea. Ambapo Jasmine Mwalami ameshitakiwa katika mahakama ya wilaya ya Ruangwa.

 


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...