Thursday, June 17, 2021

Serikali ya Ufaransa yatangaza mpango wa kuondoa ulazima wa barakoa na marufuku ya kutoka nje


Baada ya kupungua kwa idadi ya kesi za maambukizi ya corona (Covid-19) huko Ufaransa, imetangazwa kuwa sheria ya ulazima wa kuvaa barakoa katika maeneo ya wazi itaondolewa kuanzia kesho, isipokuwa kwa hali maalum, na marufuku ya kutoka nje usiku itaondolewa kuanzia Juni 20.

Waziri Mkuu Jean Castex, alizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri na kutangaza kwamba wastani wa idadi ya kila siku ya kesi za maambukizi kwa siku 7 zilizopita imepungua hadi 3,200.

Akisisitiza kuwa hakuna wasiwasi juu ya janga hilo katika mkoa wowote wa Ufaransa, Castex alikumbusha kuwa zaidi ya watu milioni 30 wamepewa dozi ya kwanza ya chanjo hadi sasa.

Akielezea kwamba sheria ya ulazima wa barakoa katika maeneo ya wazi itaondolewa kuanzia kesho, isipokuwa hali malum ya maeneo ya watu wengi, viwanjani na masokoni, Castex alieleza kuwa ni muhimu kuendelea kuvaa barakoa katika maeneo yaliyofungwa.

Castex pia alitangaza kwamba marufuku ya kutoka nje iliyowekwa kati ya 23.00-06.00 itaondolewa kuanzia tarehe 20 Juni badala ya tarehe 30 Juni.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...