Ndege aina ya MiG-29 ya Kikosi cha Wanajeshi wa Bulgaria ilianguka Cape Shabla kanda ya Bahari Nyeusi.
Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Bulgaria, ilielezwa kwamba ndege hiyo aina ya MiG-29, ambayo ilifanya safari ya mafunzo ndani ya wigo wa zoezi la kijeshi, ilipoteza mawasiliano mwendo wa saa 00:45.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa ndege hiyo ilianguka maeneo ya Cape Shabla katika kanda ya Bahari Nyeusi.
Katika taarifa hiyo ambayo haikutoa maelezo juu ya hali ya rubani, ilibainika kuwa juhudi za utaftaji zinaendelea.
Waziri Mkuu wa Bulgaria Stefan Yanev na Waziri wa Ulinzi Georgi Panayotov walikwenda kutembelea eneo la ajali.
Ndege iliyoanguka ilikuwa ikishiriki "Zoezi la Kijeshi la Shabla 2021 la Kimataifa".
Zoezi hilo, ambalo lilianza Juni 7 na litadumu hadi Juni 11, linahudhuriwa na ndege kutoka Marekani , Serbia na Bulgaria, na kujumuisha wanajeshi 1,500.
Kutokana na kuzuka kwa ajali ya ndege, shughuli za zoezi hilo zilisitishwa.
