Mwanaume anapoiingia katika ulimwengu wa mahusiano ya kimapenzi ni lazima mwanaume huyo atakutana na wanawake wenye tabia tofauti tofauti, ni miongoni mwa tabia za wanawake walio wengi katika mahusianao ni pamoaja na:
Mwanamke asie na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke ambaye hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo makusudi huku akiwa ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema umuogope sana.
Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganisha watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.
Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupita kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kugeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.
Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.
Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Kwanza aina hii ya mwanamke niwakumuogopa sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.
Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au laah! Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi ( Kukusaliti). Kwahiyo kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
