Friday, June 11, 2021

Merkel atahadharisha, corona bado haijaondoka kabisa


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametahadharisha kwamba janga la corona bado halijaondoka kabisa licha ya kuridhika juu ya kuundelea kupungua kwa idadi ya maambukizo. 

Kansela Merkel amesema hatua za kudhibiti maambukizo zilizochukuliwa tangu wakati wa Pasaka zimechangia katika kupungua kwa idadi ya watu wanaoambukizwa lakini amesisitiza tahadhari na amesema kuwa janga la corona bado halijatoweka.

 Amesema bado pana hatari kutokana na virusi vipya aina ya Delta vilivyobainika nchini India na kuenea pia nchini Uingereza. 

Shughuli nyingi zimeanza kufunguliwa tena nchini Ujerumani lakini matukio ya kuwaleta pamoja watu wengi bado hayajaruhusiwa.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...