Friday, June 4, 2021
Dkt. Mahenge Aipongeza Tarura Kuanza Kutumia Mfumo Wa Kielektroniki Wa Ukusanyaji Mapato “Termis”
Na. Bebi Kapenya
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe Dkt. Binilith Mahenge amepongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ujulikanao kama "TARURA e-Revenue Management Information System" (TeRMIS) katika Mkoa wa Singida.
Hayo yamejiri wakati wa kikao kazi kilicholenga kuwapatia mafunzo viongozi wa Mkoa wa Singida wakiwemo Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa juu ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ujulikanao kama "TeRMIS".
Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa lengo la mfumo ni kuboresha ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatakayosaidia maendeleo na maboresho ya miundombinu ya barabara, pia mfumo unalenga kumpunguzia mtumiaji wa maegesho kero ya kudaiwa ushuru kwani mteja atalipa mwenyewe kwa kutumia mtandao wowote wa simu ya mkononi, au kupitia Tawi la Benki ya NMB na CRDB au kupitia kwa Mawakala.
"Nitumie fursa hii kuwapongeza TARURA kwa kuleta mfumo huu katika Mkoa wetu kwani mfumo utaleta tija katika ukusanyaji mapato ya Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi", alisema Dkt. Mahenge.
Aidha, Dkt. Mahenge amewataka TARURA kuhakikisha elimu ya matumizi ya mfumo inafika kikamilifu kwa wananchi ili wawe na uelewa wa pamoja ili kuepusha malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi.
Pia, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kupokea mabadiliko hayo na kuanza kulipa wao wenyewe Ushuru wa Maegesho ili kuepuka adhabu na faini zisizo za lazima.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mhe. Juma Kilimbah ameipongeza TARURA kwa kuanza kutumia mfumo huo kwani mapato ya Serikali yataongezeka kwakuwa kwa kutumia mfumo huo unalipa moja kwa moja serikalini na mapato hayo yatasaidia kuboresha miundombinu ya barabara katika Manispaa ya Singida.
Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji Mapato yaani "TARURA e-Revenue Management Information System" (TeRMIS) unaosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeanza kufanya kazi katika Mkoa wa Iringa na Singida na unatarajia kusambazwa nchi nzima.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...