Friday, June 4, 2021

ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA HAI, OLE SABAYA ASOMEWA MASHTAKA 6 , LIMO LA UHUJUMU UCHUMI


Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, (wa kwanza upande wa kulia waliochuchumaa) akiwa na wenzake Mahakamani
**
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, na wenzake leo Juni 4, 2021, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka sita likiwemo shtaka la uhujumu uchumi.

Mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao ni pamoja na uhujumu uchumi, kuongoza magenge ya kihalifu, kuomba na kushawishi kupewa rushwa na unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Mshtakiwa huyo na wenzake waamekosa dhamana na kurudishwa rumande hadi Juni 18, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Sabaya na wenzake walifikishwa kwenye Mahakama hiyo leo majira ya saa 7:00 mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa TAKUKURU.

Chanzo - EATV
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...