Saturday, May 22, 2021

Waziri Ummy aunda tume, Kero za wafanyabiashara Kariakoo

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ameunda time huru ya kuchunguza kero na malalamiko ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo na kutoa siku 14 kukamilika kwa uchunguzi huo

Ameunda tume hiyo leo mara baada ya kuongea na wafanyabishara wa Soko hilo katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi na kusikiliza changamoto za wafanyabishara wa Soko hilo , Jijini Dar-es-salaam

Waziri Ummy amesema kuwa baada ya kuwasiliza wafanyabiashara hao amegundua kuwa lipo tatizo katika soko hilo ambapo amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa mahusiano mazuri kati ya wafanyabishara na menejimenti ya ya shirika la masoko la kariakoo, uwepo wa tuhuma za rushwa kwa baadhi ya viongozi wa Soko, tozo za kubwa la kodi na uwepo wa madalali wa vigoli pamoja na uwepo wa ubadhilifu wa fedha za mali za Shirika la Masoko ya Kariakoo.

Ameiagiza Tume hiyo kuhakikisha inapitia kwa kina malalamiko yaliyowasilishwa na wafanyabiashara hao ili yaeze kupatiwa ufumbuzi na Serikali kwa wakati na kufanyiwa uamuzi utakaosaidia kulipeleka taifa mbele katika kuhakikisha wafanyabishara wanafanya biashara zao katika mazingira mazuri kwa gharama zinazokubalika na Serikali

Akizungumzia uwepo wa madalali Waziri Ummy amesema kuwa kuna wapo madalali waliojimilikisha vizimba na vigoli katika soko hilo ambapo wanawapingisha wafanyabiashara wadogo kwa gharama kubwa hali hii inarudhisha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha watu wake wanapata maeneo ya kufanyia biashara ili kujikwamua kimaisha na kujiongezea kipato.

Aidha, ameiagiza Timu huru ya uchunguzi kuishauri Serikali kama upo umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa Shirika la Masoko ya kariakoo kwa kipindi cha wakati wa sasa kulingana na mabadiliko ya kisanyansi na Teknolojia.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...