Watu wasiojulikana wameshambulia kwa silaha gereza lingine katika jimbo la Abia la Nigeria.
Kulingana na habari katika vyombo vya habari vya kitaifa, wafungwa wengi walitoroka wakati gereza hilo lilipokuwa likiteketezwa katika shambulizi hilo katika mkoa wa Bende.
Mnamo Aprili 6, wafungwa 844 walitoroka na magari 50 yalichomwa moto katika shambulizi la gereza huko Owerri mji mkuu wa jimbo la Imo
Mashambulizi kama hayo hufanywa mara kwa mara na kundi linalojitenga la Biafra (IPOB) kusini mwa Nigeria.
