Friday, May 7, 2021

Tetesi za Soka Ulaya Kimataifa leo

Barcelona wameanza mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, ambayo mkataba wake Manchester City unamalizika msimu huu. (Sky Sports)


Manchester United wamefuzu kwa fainali yao ya kwanza chini ya ukufunzi wa Ole Gunnar Solskjaer lakini walipoteza rekodi yao ya kutoshindwa mechi saba katika mchezo wa kuburudisha wa Ligi ya Uropa.


Kuteuliwa kwa Jose Mourinho kama mkufunzi wa Roma msimu ujao huenda kukamfanya kiungo wa kati wa Italia Lorenzo Pellegrini, 24, kuhamia Liverpool, baada ya meneja wa klabu hiyo kuonesha nia ya kuwaleta wachezaji aanaowajua, miongoni mwao mchezaji wa kimataifa wa Serbia na Manchester United Nemanja Matic, 32. (Mirror)


Mourinho pia ana matumaini ya kuungana tena na kipa wa Manchester United na Uhispania David De Gea, 30, baada kuchukua usukani Roma. (Todofichajes - kwa kihispania)


Wachezajiwa Real Madrid wanahofia meneja wao Mfaransa Zinedine Zidane, 48, "amechoka na kukasirika" na huenda akaondoka klabu hiyo kabla ya kukamilisha mwaka wa mwisho katika kandarasi yake msimu huu wa joto. (Goal)


Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Brighton Yves Bissouma, 24, huku Tottenham, West Ham na Everton pia zikimuulizia. (Express)

Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Mali Bissouma, baada ya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka Declan Rice, 22 wa West Ham'. (Star)

 


Manchester United wameambiwa mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mreno Andre Silva, 25, anagharimu £35m msimu huu. (Express)


Chelsea itawauza walinzi wake kukusanya fedha za kuwanunua wachezaji wengine, wanaopigiwa upatu kuondoka Stamford Bridge ni Marcos Alonso, 30, na Emerson Palmieri, 26. (Goal)


Atletico Madrid wanamnyatia kiungo wa kati wa Barcelona aliye na umri wa chini ya miaka 21-Mhispania Riqui Puig msimu huu wa joto. (Fichajes - in Spanish)


Barcelona na Paris Saint-Germain wanamfuatilia mlinzi wa Monaco kutoka Brazili Caio Henrique,23. (UOL - in Portuguese)

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...