Tuesday, May 18, 2021

Rais Samia "Sheria ya PF3 Itazamwe Upya, Watu Wanakufa Tumepoteza Watu Wengi"



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka jeshi la polisi kuangalia upya kipengele cha PF.3 kwa watu wanaopata ajali kwa sababu kinasababisha watu kupoteza maisha.


Rais Samia amesema hayo leo Mei 18, 2021 wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha jeshi la polisi kilichopo kilichopo katika Bohari Kuu ya Jeshi la Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam na kuagiza kuwa mtu anapopata ajali, kipaumbele cha kwanza kiwe ni kupatiwa matibabu, kisha hatua za kipolisi zitafuata.



"Kuna wanaopata ajali wanaumia kwa viwango tofauti tofauti mwingine anapoumia anapofika hospitali inabidi ashughulikiwe haraka, lakini sheria yetu hawezi kuhudumiwa mpaka iende PF3 watu wanafia pale hospitali, hii sheria muiangalie. Mtu akipata ajali apate huduma kwanza kisha mambo mengine yaendelee, tumepoteza watu wengi (wanafariki) sababu ya PF 3.



"Kiwanda hiki cha ushonaji cha Jeshi la Polisi, Kurasini Dar es salaam, kitazalisha sare za Askari, nimeoneshwa uniform za awali ni nzuri mno, niviombe na Vikosi vingine vya ulinzi vije vishone hapa, tukuze zaidi Kiwanda cha Polisi," amesema Rais Samia


Aidha, Rais Samia amelitaka jeshi la polisi kujielekeza zaidi kutoa elimu badala ya kutumia sheria zao kutoza faini. Pia amelitaka jeshi hilo kuwa na mfumo utakaosomeka nchi nzima na kuonesha makosa ya madereva, na yakifika kiwango fulani, dereva anyang'anywe leseni.


Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...