Tuesday, May 11, 2021

Putin awasilisha rasimu ya sheria ya kuitowa Urusi mkataba wa Open Skies


Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amewasilisha bungeni rasimu ya sheria ya kuitowa nchi yake kwenye mkataba unaoziruhusu nchi kurusha ndege kwenye anga za mataifa mengine kwa kutowa taarifa ya muda mfupi kwa lengo la kufuatilia shughuli za kijeshi. 

Hatua hiyo ya Putin inafuatia uamuzi wa Marekani chini utawala wa Trump kujitowa kwenye makubaliano hayo ya ulinzi ya baada ya Vita Baridi. 

Mwezi Januari mwaka huu, Urusi ilitangaza kwamba ingelijiondowa kwenye mkataba huo, ambao pia umesainiwa na nchi nyengine zaidi ya 30 ulimwenguni.

 Mkataba huo uitwao Open Skies ni moja kati ya mingi ambayo Marekani ilijiondowa chini ya utawala wa Trump. 

Mnamo mwezi Februari, mrithi wa Trump, Joe Biden, aliuongezea muda wa miaka mingine mitano mkataba pekee uliokuwa umesalia miongoni mwa mikataba ya kupunguza mashindano ya silaha, uitwao New START, ambao unahusu silaha za nyuklia.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...