Friday, May 21, 2021

Mwanamke raia wa Rwanda akiri kuwasajili wasichana kwenye kundi la waasi





Angeline Mukandutiye, mwanamke pekee katika kundi la Wanyarwanda 21 wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi, amekiri kuwasajili wasichana kwenye kikundi cha upinzani cha Rwanda ambacho kilifanya operesheni katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kikundi hicho ni pamoja na Paul Rusesabagina, mtu aliyeoneshwa kama shujaa katika filamu ya 2004 ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Bi Mukandutiye, 70, aliwaonesha majaji katika Mahakama Kuu katika mji mkuu, Kigali, washtakiwa wenzake ambao walikuwa pamoja naye kundi la CNRD - FLN.

Mkaguzi wa zamani wa shule alikimbia Rwanda mnamo 1994 na kuchukua jukumu la kamishna anayesimamia familia na maendeleo katika CNRD-FLN.

Siku ya Alhamisi, aliiambia mahakama kwamba aliamini ''wanatafuta umoja na demokrasia nchini Rwanda lakini alikana kuhusika na mashambulizi mabaya ya mwaka 2018 na 2019.

kamishna ... mara nyingi tulishambuliwa na waasi wengine, nilifikiria kile ninachoweza kufanya na nikapendekeza kwa viongozi wetu kwamba wasichana wanaweza kupewa mafunzo ya kijeshi ili kujitetea.

"Nilihamasisha [wasichana] na walipenda. Nilitengeneza orodha ya wajitolea na kuwapa wale walioajiriwa, "aliiambia mahakama.

Alipoilizwa kuhusu idadi ya wasichana aliowaorodhesha alisema ''walikuwa wengi hilo ndilo ninaloweza kusema ''.

Mwishoni mwa mwaka wa 2019 jeshi la DR Congo lilishambulia maeneo ya waasi na kuwakamata washiriki wake wengi na familia zao. Wengi wao walirudishwa nchini mwao. Bi Mukandutiye alikamatwa wakati wa kuwasili Rwanda.

Utata juu kukamatwa kwa 'shujaa' wa filamu ya mauaji ya Rwanda.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...