Monday, May 10, 2021

Lindi watahadharishwa maambukizi ya VVU, halmashauri na tume zasaini mikataba


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wananchi mkoani Lindi wametahadharishwa wasijisahau nakushindwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI( VVU). 

Tahadhari hiyo imetolewa leo mjini  Lindi na mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga wakati wa hafla ya utilianaji saini mikataba baina ya halmashauri za Mtama, Kilwa na Nachingwea na tume ya kikristo ya utoaji huduma kwa jamii (CSSC).

Akizungumza katika ghafla hiyo ambayo ilikwenda sanjari na utambulisho wa mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama wajawazito kwenda kwa watoto, alisema wananchi hawanabudi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizo hayo.

 Alisema kuna dhana mbaya imejengeka kwamba mkoa wa Lindi hauna UKIMWI. Dhana ambayo ni hatari na haifai kuachwa iendelee.

Mkuu huyo wa wilaya ya Lindi ambae alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi kwenye hafla hiyo alisema licha ya utafiti kuonesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU katika mkoa huu kuwa kidogo, lakini siyo sababu yakutochukua tahadhari dhidi ya maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Ndemanga alitahadharisha kwamba halitakuwa  jambo la ajabu kwakiwango cha maambukizi kupanda kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 0.3 iwapo wananchi watashindwa kuchukua tahadhari kutokanana imani kwamba mkoa huu hauna UKIMWI.

Mbali na hayo, Ndemanga alitoa wito kwa wadau kuwa na mwendelezo wa miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa muda maalumu. Kwani uzoefu unaonesha kwamba  miradi mingi imekoma na kufutika baada ya kukamilika muda wa utekelezaji.

Alisema kuna kila sababu ya miradi kuwa endelevu hasa  baada ya wahisani na wafadhali kukamilisha muda wao wa ufadhili kwamujibu wa muda wa utekelezaji wa miradi hiyo. 

" Miradi hii niyawananchi. Kwahiyo hata muda wa utekelezaji unapokamilika nilazima iendelee kuwahudumia wananchi. Mradi kama huu ukikamilika muda wake haimaanishi kwamba maambukizi yatakuwa yamekwisha," alisisitiza Ndemanga. 

Kwaupande wake mkurugenzi wa programu global fund ambayo inafadhili mradi huo kupitia AMREF Health Africa, Dkt Amos Nyirenda alitoa wito kwa watu wenye uwezo wa kununua kondomu wafanye hivyo badala ya kutegemea kondomu zinazotolewa bila malipo.

Dkt Nyirenda alisema mahitaji halisi ya kondomu kwa mwaka ni kondomu milioni 260. Hata hivyo upatikanaji wake ni mdogo ikilinganishwa na na mahitaji halisi.

Halmashauri za Mtama, Kilwa na Nachingwea zitiliana saini na tume ya kikristo ya utoaji huduma kwa jamii. Mradi ambao utakelezwa kwa muda wa miaka mitatu.

 Tume ya kikristo ya utoaji huduma za jamii ni miongoni mwa taasisi tano zinazoshirikiana na AMREF kutekeleza mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU  kutoka kwa mama wajawazito kwenda kwa watoto.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...